RECIPE YA NYAMA YA NGO’MBE ILIYO WEKWA MCHAICHAI

-Je unajua mchaichai ni kiungo kizuri kwa nyama?!
Leo napenda ni share recipe nzuri sana na amazing, itakayo kuongeza ujuzi ktk mapishi ya nyama.

Mchaichai kwenye nyama unaleta ladha nzuri sana, na nyama inanukia vizuri sana. Yani ukiweka kwenye nyama hadi hamu ya kula inaongezeka, na hata ule nyama nyingi huwezi kukinai.

-Mi nimetumia nyama ya ngo’mbe, ( unaweza tumia nyama aina yoyoye) ambayo baada ya kuiwekea viungo nika ichemsha na kuikaanga kwenye mafuta machache , #shallowfriying.
.
Ni nzuri sana kama hupendi nyama ya mchuzi na vile vile hupendi nyama iliyo kaangwa kwenye mafuta mengi. #deepfyring
.
Na hivi ndivyo nilivyo pika;

Niliosha nyama na kuikata vipande vya wastani kisha nika iweke kwenye sufuria

. Nika saga viungo kwenye blender mchaichai, tangawizi, kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili mwendokasi za kijani, Nika weka maji kikombe 1. Nika Saga hadi mchanganyiko wangu ulipo kuwa laini kabisa.

Kisha nikatia chumvi kwenye nyama, na ku-mimina viungo kwenye nyama, nikaweka na limao. Halafu nikachukua mwiko na kuhakikisha na mix vizuri, viungo vyangu vienee vyote kwenye nyama.

-Nikaweka sufuria jikoni, na kuwasha jiko. Nika chemsha nyama hadi maji yalipo kaukia, Nika igeuza na mwiko na kuongeza maji tena na mafuta kiasi.


Kisha nika acha ichemke hadi, hadi maji yakaukie kabisa, yakabaki mafuta tu.

Hapo nikawa naigeuza kila baada ya dk kadhaa, halafu naacha ijikaaange kwenye mafuta. Naigeuza tena, na naacha ijikaaange, Nika endelea hivyo hadi ilipo kuwa brown. Hapo ikawa tayari kwa kuliwa.


Si tulikula na yellow fried rice, ila unaweza kuila na vitu vingi ugali, ndizi mzuzu, mihogo ya kukaanga, chipsi, pilau bubu, tambi nk.

@eunicemahundi

karibu

Share kwenye comments wewe hii nyama ungeila na chakula gani, kiungo Gani ungeongeza na kipi ungepunguza.
.
Usisahau ku-subscribe #malkiawajikoblog na pia kushare recipe hii na uwapendao.
.
Check pia recipe ya 👇

JINSI YA KUANDAA MISHIKAKI YA NGO’MBE [ ORANGE RED MISHIKAKI]

Design a site like this with WordPress.com
Get started