-Dagaa ni mboga simple na nzuri sana, hasa kula na ugali. Inaingia kwenye top ten, ya mboga nazoi zipenda kula na ugali.
Na hapa Leo nashare dondoo chache ila muhimu uweze kuongeza maarifa ktk upishi wa dagaa.

1. Nunua dagaa wenye quality ya juu; hawa huwa na size kubwa, wasafi, wamekauka vizuri, hawana uvundo, hawana mawe/mchanga wala wadudu. Zingatia sana hili, dagaa wakiwa na quality nzuri hata ukiwapika ladha huwa nzuri na hupati shida kwenye kuwaandaa.
Yani hata ukipika chukuchuku ukaweka chumvi, ndimu na pilipili watu watakula hadi ushangae.
.
Dagaa wenye quality mbovu, kwenye mapishi ni mtihani maana huwa Wana harufu ya uvundo, halafu huwa wengi wamesha haribika, michanga kibao utaosha hadi dagaa wana legea, na ukipika hata uweke Nini ladha yao haina ushirikiano.

2. Viungo viwe vya wastani: mfano ukiweka katangawizi, saumu, ndimu, chumvi na pilipili inatosham. Viungo visizidi vitano, ili dagaa wabaki na ladha yao original.

3.Dagaa usizinyime nyanya: ukiamua kupika rosti dagaa au dagaa wa mchuzi. Weka nyanya za kutosha ladha ya dagaa itazidi kuwa nzuri.
Ukiwa hupendi nyanya pika dagaa wa kukaanga. Nyanya hata uweke nyingi kwenye dagaa hakita haribu ladha ya dagaa au kupoteza ladha ya dagaa. Ila itafanya ladha ya dagaa izidi kunoga.

4.Mboga mboga nzuri za kumix kwenye dagaa ni bamia , kabichi na nyanya chungu. Hata ukiweka nyingi hazina shida, maana zina tabia ya kupokea ladha ya dagaa sio kufanya dagaa wapoteze ladha yao.
Hoho, karoti na bilinganya ukiweka kwenye dagaa ziwe kidogo tu, ukiweka nyingi zina tabia ya kuifunika ladha ya dagaa.

5. Ukiamua kukaanga dagaa, tumia mafuta fresh sio yaliyo Kaa sana na kutumika muda mrefu. Utaharibu ladha ya dagaa.
.
Zingatia hizo dondoo zita kusaidia sana kwenye mapishi ya dagaa, watoke wazuri na watamu.
Pls share na wengine nao wajifinze , pia like na comment. Subscribe ili nikiwa napost usipitwe.
.