➡️Karibuni, juice ya passion na karoti. Hii nime tengeneza jana, kwa ajili ya my girls wamekunywa baada ya kutoka shule.

➡️Baada ya kuosha karoti na mapassion, nikakata kata karoti na kuweka ktk blender, nika weka pia na passion. Nika weka na maji glass 3 kwenye blender, kisha nika blend hadi ilipokuwa tayari. Nikachuja na kuweka sukari kiasi.

➡️Kisha nikachukua glass nikaweka ice cubes na mint, nikamimina juice ktk glass nikaweka na mirija na hapo juice yetu ikawa tayari kwa kunywa.

➡️Karibu kwenye comments ushare uzoefu wako chochote kile kuhusu juisi ya passiona na karoti, pia maswali na mengineyo.
Hbr mbona mbegu za passion ukisagia pamoja juice inakuwa chungu mwishoni?
LikeLike
Passion mbona ukisaga laziima usage na mbegu, na huwa haiwi chungu. Karibu kuchunguza labda Kuna kitu kinasababisha, au ukitengeneza tengeneza ya kunywa siku moja iishe isilale uone kama itakuwa chungu. Check na ma passion quality yk ikoje.
LikeLike