➡️ Karibuni maandazi, hapa na share recipe yangu ya maandazi, ambayo itakusaidia uweze kutengeneza maandazi mazuriii kwa urahisi na kuepuka kero ya kutafuta vitafunwa au kula mikate kila siku 😀.

➡️Recipe ya maandazi hii hapa 👇🏿
.
Mahitaji
Ngano kilo1, Mafuta lita 1, Sukari 200 gramu, Maji robo lita, Hamira vijiko 4 vidogo.

Jinsi ya kutengeneza
➡️ Weka maji kwenye bakuli yawe ya uvuguvugu kisha tia hamira koroga mpaka iyeyuke, kisha tia unga wa ngano katika bakuli kubwa ya kukandia, kisha tia sukari na mafuta kama vijiko vinne vikubwa katika unga, kisha tia maji uliyochanganya na hamira, anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika vizuri utengeneze donge moja kubwa.


Kisha baada ya kukanda acha kama dakika kumi na tano ngano yako, baada ya hapo ndio usukume na kukata shepu za maandazi unazotaka, acha yaumuke kama masaa mawili kisha kaanga. Unaweza kunywea chai maandazi au kinywaji chochote upendacho.


karibu kwenye comments kwa chochote kuhusu maandazi, pia usisahau ku follow blog ya malkia wa jiko, uweze kupata email kila napo post.
Najifunza
LikeLike
Karibu dear 😍🙏
LikeLike
Karibu sn dear
LikeLike
Mimi maandazi yangu yanakua na space kwa ndan japo nakata manene huwa sipendi nikiwa nachoma andazi lipande kama puto nifanyeje?
LikeLike
wakati wa kukakata usiyafanye membamba sana na weka amira ya wastani na usiache yaumuke muda mrefu sn
LikeLike
Mbpna kwenye maelekez yako hakuna cardamom na baking powder
LikeLike
Mimi huwa siweki, maandazi naweka hamira tu.
LikeLike
Hbari, hauna pdf ya mapishi?
LikeLike
Sina
LikeLike
I like it
LikeLike
thanks
LikeLike
Haya mandazi siyo lazima backing powder au chapa mandazi????
LikeLike
ndio siyo lazima, mimi siwekagi baking powder au chapa maandazi ni hamira tu inatosha, Na yanatoka vizuri sana ladha hata muonekano pia
LikeLike