JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KUSUKUMA

➡️ Chapati za kusukuma; huwa napenda sana, ni tamua na hazina usumbufu wowote ktk kupika. Na uzuri chapati unaweza ukala wakati wowote iwe asubuhi, mchana au jioni. Hapa na -share recipe yangu ya chapati hope itawasaidia wengi;


Chapati recipe
Mahitaji
– ngano 1/2 kg
– mafuta 1/4 L
-chumvi kijiko kidogo 1
– maji 400 m/l


Jinsi ya kutengeneza

Weka maji kwenye kibakuli (400 M/l) yawe ya uvuguvugu kisha tia chumvi na koroga vizuri ichanganyike.
Tia unga wa ngano katika bakuli kubwa ya kukandia, kisha tia mafuta kama vijiko vinne vikubwa katika unga. Kisha tia maji katika unga na anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika vizuri utengeneze donge moja kubwa. Ukimaliza anza kutengeneza vidonge vidogo vya duara, kama kwenye picha kisha unavipanga kwenye kibao.

Kisha unachukua moja moja unasukuma, unaweka frying pan yako jikoni ukipata moto unaweka chapati, unaigeuza pande zote mbili ipate moto kisha unaweka mafuta unakaanga upande wa juu ukiwa tayari unageuza upande mwingine unaweka mafuta unaikaanga ukiwa tayari unatoa, unafanya hivyo mpaka zote zinaisha. 👇🏿
.

Chapati zako unaweza kula na chai, juisi au mchuzi wa nyama, maharage, mboga za majani au chochote utakachopenda.
.

➡️Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

6 thoughts on “JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KUSUKUMA

Leave a reply to eunicemahundi Cancel reply

Design a site like this with WordPress.com
Get started