JINSI YA KUTENGENEZA MEATBALLS

-Leo napenda nielekeze kitu kingine muhimu, jinsi ya kutengeneza meatballs.
-Meatballs ni nyama ya kusaga iliyo tengenezwa ktk umbo la duara. Kama unavyoona kwenye picha Ni rahisi kutengeneza na ni nzuri sana kwa kula (ukizikaanga au rosti) na tambi, mashed potatoes au chipsi nk.

meatballs za kukaanga

Mahitaji
-Nyama ya kusaga kilo 1
-Breadcrumbs nusu kikombe
-mayai 2 makubwa mabichi
-Kitunguu saumu na tangawizi kijiko 1kikubwa
-chumvi kijiko kidogo 1

Jinsi ya kutengeneza

1.Naweka nyama kwenye bakuli kubwa, kisha naweka na breadcrumbs, mayai na kitunguu saumu, tangawizi na chumvi. Kisha nikaanza kumix kwa kutumia mikono hadi vyote Kwa pamoja vika changanyika vizuri.

2.Kisha nachota na kijiko kikubwa kimoja kutoka kwenye mchanganyiko wa nyama, na nikatengeneza kiduara kutumia mkono ili kupata meatball, nikaendelea kutengeneza vingine hadi nyama yote ilipo isha

3.Meatballs unaweza zipika hapo hapo baada ya kutengeneza au ukaweka kwenye freezer Kwa matumizi ya baadaye. Unaweza kuzipika kwa kukaanga, kuoka au kuunga na nyanya.

meatballs na tambi

-Hivyo ndio jinsi ya kutengeneza meatballs, rahisi kabisa na hazina kazi kuzipika mi napenda kuzikaanga na mara moja moja kuzipika rosti kwa ajili ya tambi. Usisahau ku like, share na kuacha comment. Endelea kutembelea #malkiawajiko blog kujifunza mapishi na dondoo za jikoni.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started