JINSI YA KUTENGENEZA SPRING ROLLS

-Spring rolls ni kitafunwa kizuri na mimi napenda sana kukitengeneza, maana kinaenda na kinywaji chochote kile moto au baridi.Spring rolls unatengeneza kwa kutumia manda kama zile tunazo tumia kwenywe sambusa, na ndani unaweka nyama ya kusaga au mbogamboga kisha unazifunga ktk shape ya cylinder kama unavyoona ktk picha halafu unazikaanga ktk mafuta.

Hapa nitakuelekeza jinsi ya kuzitengeneza, Mahitaji ni kama ifuatavyo:

nyama ya kusaga kl 1.manda (kama 30 zilizo ktk umbo la mraba.vitunguu maji vikubwa 4.karoti kubwa 4.chumvi kjk cha chai 1.tangawizi na kitunguu saumu (iliyo sagwa kjk 1 kikubwa). Mafuta ya kupikia lt 1

Jinsi ya kutengeneza

1.Nyama ya kusaga niliweka kwenye chujio na kuiosha kisha nikaweka kwenye frying pan, Bila kuweka mafuta,[ maana nyama yenyewe ilikuwa na mafuta] maji yalipo kaukia, kisha nikaweka karoti, vitunguu na kitunguu saumu, na tangawizi nikaendelea kuikaanga na mafuta yake yenyewe hadi ilipo kuwa tayari, nikaitoa ni kaacha ipoe.

2 Ndio nikaanza kuzifunga. Spring rolls. Nachota nyama kijiko 1 kikubwa cha chakula, naweka ktk manda kisha nafunga( angalia jinsi ya kuzifunga ktk picha) nafunga hadi zote ziishe.

3.Nikimaliza nachukua chache nakaanga kama nahitaji kula siku hiyo hiyo.

4.Nyingine naweka ktk freezer bags kisha nahifadhi ktk freezer, nikihitaji natoa nakaanga.Note; jinsi navyotengeneza spring rolls ndivyo hivyo hivyo navyo tengeneza sambusa tofauti ni ufungaji maana umbo la sambusa na spring rolls tofauti.Asante kwa kutembelea blog ya malkia wa jiko, usisahu ku like, share na kuacha comment. Karibu

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started