
➡️ Chicken tenders, hizi niliwapikia jana usiku my girls, ni nzuri sana na hasa kwa watoto, usiwanyime wanao uhondo wapikie #chickentenders recipe hii hapa ⤵️
Chicken tenders, ni nyama ya kuku isiyo na mifupa, na unatumia nyama ya kidari cha kuku ambayo huwa nyeupe kabisa haina mafuta kama mapaja.

Mi nimetumia vidari viwili, baada ya kusafisha na kumuandaa kuku, nikatoa nyama ktka kidari, na kuikata vipande vya ukubwa wastani nikaviwekea chumvi kidogo sn, kitunguu saumu, tangawizi, curry powder kidogo, na limao. Kisha nikaweka nyama kwenye fridge kwa nusu saa viungo vikolee.
Baada ya hapo nikatoa nyama kutoka kwenye fridge, nikavunja yai moja na kuli piga piga kisha nikaliweka ktk nyama na nikamix vizuri nyama na yai kwa kutumia mkono. Nikaweka mafuta ktk frying pan, na kuibandika jikoni yalipo pata moto nikawa natoa kipande kimoja cha nyama na kukichovya kwenye unga wa ngano mkavu kisha naweka kwenye mafuta, na kuvikaanga hadi vikaiva na kubadilika rangi kama unavyo iona.
Hizi chicken tenders walizila na chipsi, salad ya tango na nyanya na juice ya embe. #itwasdelicous.
.
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 natuma kwenye email.
Whatsap 0752 741 831.