JINSI YA KUTENGENEZA PILIPILI YA EMBE

➡️Pilipili ya embe: Hii ni pilipili nzuri sana unaweza kula na vitu vingi nyama choma, chipsi, pilau, ndizi choma nk.


➡️Nimeweka -embe 1 bichi dodo kubwa, -pilipili mbuzi nyingi, -kitunguuu saumu 1, -tangawizi kiasi,
-Chumvi kijiko 1 kidogo
-majani ya rosemary kidogo
-na curry powder kidogo.

➡️Nimemenya embe na kuli katakata, nikamenya saumu,tangawizi, nikakatakata pilipili kisha nikaweka kila kitu ktk blender nikaweka pia na rosemary, na curry powder, vinegar kidogo na chumvi nika blender hadi mchanganyiko wangu ulipo kuwa laini, ila sikutaka uwe laini sana.


➡️Baada ya hapo nikweka mafuta jikoni yalipo pata moto, nika mimini pilipili yangu ktk mafuta na kukaanga kwa dk kadhaa, kidha nikazima jiko. Na kuacha pilipili ipoe. Halafu tukaila ni pilipili nzuri sana 😍.

Usisahau ku like, comment na ku share.

Design a site like this with WordPress.com
Get started