➡️Kashata za karanga, hizi ni simple kupika na nzuri sana kunywea kahawa mida ya jioni jioni.

➡️Hapa nimetumia vitu viwili 2 kupika hizi kashata, karanga na sukari. Karanga zilikuwa zimesha kaangwa na kutolewa maganda, kama robo kl na sukari nayo kama robo.

➡️Niliweka friying pan jikoni, ilipo pata moto nikaweka sukari nikaacha hadi iyeyuke kabisa na kuwa rojo, nikaweka karanga na kumix vizuri zichanganyike na sukari, nikaacha kama dk 2 tatu sukari na karanga zishikane vizuri kisha nikazima jiko.

Nikachukua ubao na kuupaka mafuta, kisha mchanganyiko wa karanga na sukari nikaumwagia juu ya ubao, kisha nika tengeneza vizuri kutumia mti wa kusukumia chapati, umbo zuri la duara. Nikaacha kidogo upoe kisha nikachukua kisu na kuanza kukata mistari ya wima na ulalo kupata kashata. Na hapo kashata za karanga zikawa tayari. Nika zila na kahawa.
