Wali manjano ni mtamu sana na rahisi kupika, mi napenda sana kuupika hasa pale napokuwa nimechoka kula wali mweupe, na hapa nashare recipe yake mjifunze.

Mahitaji
mchele kilo 1
tui la nazi zito kikombe kimoja
tui jepesi lita 1
kitunguu saumu kilicho sagwa vijiko 2 vikubwa
njegere zilizo chemshwa kikombe 1 kidogo
curry powder vijiko 3vikubwa na manjano vijiko 3 vikubwa
chumvi kijiko 1 kidogo
mafuta ya kupikia vijiko 2 vikubwa

Jinsi ya kupika
Baada ya kuosha mchele uache uchuje maji. Kisha bandika sufuria jikoni, weka mafuta yakipata moto tia kitunguu saumu, kikaange hadi kianza kunukia, tia binzari manjano na cuury powder na endelea kukaanga kwa dk kama 1, weka , mchela na mix vizuri hadi uone mchele unaanza kuwa wa njano. Tia chumvi na uweke jepesi. funika na acha lichemke hadi likaukia, hapo punguza moto na weka njegere, weka pia na tui zito kisha mix vizuri funika sufuria na acha hadi tui zito nalo likaukia, hapo toa wali wako jikoni na weka kwenye oven set moto wa wastani na acha wali ukauke hadi uone umechambuka vizuri, hapo utakuwa tayari kuliwa.

Wali manjano unafaa kuliwa kwa mboga yoyote ile unayo penda, si tuli ula na nyama na cabbage ya kukaanga. karibu ku like, share na comment.