Breadsticks; au viite viji- mkate hii nilitengeneza jana usiku na leo asubuhi ndio imetumika kama kitafunwa cha watoto wakati wa chai. Menu ilikuwa breadsticks + mayai ya kuchemsha + spice tea. Breadsticks ni rahisi sn kutengeneza pia ni tamu. Recipe hii hapa 👇🏿,
☕️🍞

Mahitaji
-Ngano robo kl
-sukari vijiko vikubwa 5
-chumvi kijiko cha chai 1
-mafuta vijiko vikubwa 4
-yai 1
-maji ya uvuguvugu kikombe 1 (mug)
-hamira vijiko vya chai 2
🍞
Jinsi ya kutengeneza
- Weka hamira kwenye maji na ikoroge ichanganyike vizuri kisha weka pembeni.
- weka unga kwenye bakuli, weka na sukari, chumvi, na mafuta vijiko 3. Mix vizuri na mwiko, kila kitu kichanganyike – Kisha tia maji kidogo kidogo kwenye bakuli huku unaanza kukanda unga.
- Kanda unga hadi uwe laini kisha uache uumuke km dk 60 au (zaidi kutegemea na aina ya unga na hamira uliyo tumia)
- Ukisha umuka, weka donge la unga kwenye kibao cha chapati, Kisha sukuma donge la unga kutengeneza duara moja kubwa ( km unavyo sukuma chapati)
- Kisha kwa kutumia kisu kata vipande vyembamba virefu Kama unavyo ona size za hizo breadsticks.
- Chukua chombo cha kuokea na kipake mafuta kijiko 1 kikubwa
- Halafu zipange breadsticks kwenye chombo cha kuokea, vunja yai weka kwenye bakuli lipige pige hadi litoe povu, Kisha kwa kutumia pastry brush, paka yai juu ya breadsticks

– Kisha ziweke ktk oven na oka kwa dk 15, moto weka 190 degrees.
🍞
Ukitengeneza uje kutupa mrejesho.
👇🏿
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.
.