JINSI YA KUPIKA PIZZA YA NYAMA YA KUSAGA

Jana jumamosi nilipika pizza ya nyama ya kusaga, my girls wanapenda sana pizza huwa napenda kuwapikia pizza za viti tofauti tofauti (kuku, sausage, ntama kusaga)nk. Hapa nashare recipe ya pizza ya nyama ya kusaga.

Mahitaji

Tomato paste(nyanya ya pakti) pakti 1, -nyanya 2, -hoho 1, -nyama ya kusaga (kibakuli 1 kidogo) iwe ime chemshwa-karoti 1 (katakata ktk umbo la duara) , -baby onions 4 (au kitunguu cha kawaida) -ngano robo.

➡️ Kwanza nilianza kutengeneza pizza base, (ngano una isukuma kutengeneza shape ya chapati, kama unavyo ona ktk picha). Nilitumia ngano robo, chumvi kijiko cha chai kidogo, mafuta vijiko 4, hamira kijiko kidogo 1, na maji kikombe 1. Niliweka hamira kwenye maji nika mix hadi ikayeyuka vizuri, nikaweka ngano ktk bakuli na chumvi na mafuta kisha nikaweka maji na kukanda unga hadi ulipo kuwa tayari, nikauacha uumuke kwa nusu saa.

➡️ Baada ya ngano kuumuka, nikaisukuma na kutengeneza pizza base.- Kisha nikapaka tomato paste juu ya pizza base, halafu nikaweka nyanya, hoho, karoti, nyama ya kusaga na baby onions. Hapo pizza ikawa tayari kwa kuoka. Nikaweka pizza ktk oven kwa dk kama 10, niliset oven 200°c . Na pizza ikawq tayari kuliwa, karibu.

Karibu kwenywe comments ushare uzoefu chochote kuhusu pizza. Maswali, usisahau ku like na ku subscribe 🤗.

Design a site like this with WordPress.com
Get started