➡️Karibuni, juice ya passion na karoti. Hii nime tengeneza jana, kwa ajili ya my girls wamekunywa baada ya kutoka shule.

➡️Baada ya kuosha karoti na mapassion, nikakata kata karoti na kuweka ktk blender, nika weka pia na passion. Nika weka na maji glass 3 kwenye blender, kisha nika blend hadi ilipokuwa tayari. Nikachuja na kuweka sukari kiasi.

➡️Kisha nikachukua glass nikaweka ice cubes na mint, nikamimina juice ktk glass nikaweka na mirija na hapo juice yetu ikawa tayari kwa kunywa.

➡️Karibu kwenye comments ushare uzoefu wako chochote kile kuhusu juisi ya passiona na karoti, pia maswali na mengineyo.