VINYWAJI LAINI NYUMBANI (jinsi ya kutengeneza juisi ya rosella, juisi ya ubuyu na juisi ya ukwaju)

➡️Vinywaji Nyumbani : kuna fan wangu wa #malkiawajiko nilikuwa nachat naye . Alikuwa ana hitaji kujua juice nzuri unazo weza tengeneza nyumbani kwa urahisi bila kutumia blender. Na-share hapa kwa faida ya wengi.

➡️Hapa kuna juice aina 3, rosella juice, ubuyu juice na ukwaju juice. Hizi zote ni juice nzuri sana, rahisi kutengeneza na zina faida kwa mwilini ukinywa mara kwa mara, -kama kupunguza uzito
-kuondoa tatizo la kukosa choo
-kuondoa uchovu
-kuongeza kinga ya mwili
-kuondoa tatixo la kukosa usingizi
-kuondoa kichefuchefu
-nk

.
➡️Kama hatuja endelea niseme kitu kimoja (kipimo) muhimu, kutengeneza hizi juisi huwa natumia , nusu kilo ya rosella (kavu)/ukwaju/ubuyu kwa lita mbili za maji. Kwa matumizi ya nyumbani, hapa juice inatoka ikiwa nzito na ladha inakuwa bado strong.

rosella kavu

➡️Rosella juice: baada ya kuinunua rosella ichambue kwanza, ingawa mara nyingi zinakuwa safi tu. Na chagua zile zenye majani makubwa na yaliyo kauka vizuri.
-ukisha ichambua, weka maji kwenye sufuria, weka rosella na ichemsha hadi ichemke vizuri kabisa. Zima jiko, iache ipoe kabisa, chuja, weka sukari au asali na vanilla flavour mix vizuri. Kisha Iweke ktk fridge na iache ipate ubaridi wa kutosha hapo rosella juice itakuwa tayari kwa kunywa #enjoy 🍷. Wakati wa kuchemsha mi huwa naweka kidogo mdalasini na iliki kiduchu kwa ajili ya harufu nzuri.


➡️Ubuyu juice: ubuyu wa mbegu mi ndio nao pendelea zaidi. Maana wakati wa kununua, ni rahisi kuukagua haraka na unaweza kujua kama umekaa sana au la. Chagua ubuyu ambayo mbegu zake bado ni nyeupe, usio na taka na ambao haujafungwa kwenye mifuko.
-Chemsha maji ya moto hadi ya chemke sana. Zima jiko, kisha weka ubuyu na hakikisha ubuyu wote umezama kwenye maji, funika na mfuniko. Acha hadi maji yapoe, kisha chukua mwiko na mix vizuri kuhakikisha ubuyu wote umelainika na mbegu zimebaki tupu. Chuja na weka sukari/asali weka kwenyw fridge ipate baridi, enyoy 🤗.
Mimi binti zangu juice ya ubuyu huwa wana weka vitu vingi. Wana mix na maziwa, wanaWeka tangawizi, mint leaves, vanilla. Ila mi naona vurugu tu, sijui ndio uzee😎. Mi huwa ya kwangu naweka Sukari basi.

➡️Ukwaju juice: Ukwaju chagua ambao haujakaa sana, na bei yk inakuwaga kubwa, utaona bado uko brown, soft na u navutia. Sio ulehb umekuwa mweusi, unanata na umeshikana sana.
Kama kwa ubuyu, chemsha maji yachemke hasa, zima jiko weka ukwaju funika na mfuniko. Acha hadi upoe mix vizuri na mwiko hakikisha ukwaju wote umetoka na kutengana na mbegu zake, chuja weka sukari au asali, ukipenda kamulia ndimi kidogo tu weka kwenye fridge ipate baridi na enjoy.

➡️So hope utatumia huu ujuzi kuetengeneza juisi nyumbani kwako kuenyoy na uwapendao, au hata kwa biashara.
Unaweza kushare zaidi ktk comment kuhusu hizi juisi tujifunze zaidi ❤❤.

Design a site like this with WordPress.com
Get started