JINSI YA KUPIKA KUKU WA MCHUZI (#CHICKENSTEW)

Chicken Stew (kuku wa mchuzi): huyu ni mtamu sana na uzuri anaweza kuliwa na vitu vingi na uka enjoy mlo wako. Iwe ugali, wali, pilau, ndizi za kupika, chapati na chochote utakacho penda.
.
Upishi wake ni rahisi sana, viungo vya wastani. Hapa nita elekeza jinsi ya kumpika vizuri, na utatamani uwe unapika na kula kila siku.

.
Mahitaji
Kuku 1(broiler)
Nyanya maji 4
Nyanya pakti 1
Kitunguu kikubwa kabisa 1
Garlic Ginger Paste kjk kikubwa 1
Manjano kjk kikubwa 1
Chumvi kijiko kdg 1
Limao nusu
Mafuta ya kupikia vijiko 4 vikubwa
.
Maandalizi
-Niliosha kuku na kumkatakata vipande vya wastani, Kisha nika mweka kwenye sufuria.
-Nika osha nyanya, kitunguu na katakata
-Nika oshha tangawizi, menye katakata menye kitunguu saumu. Nika twanga vyote pamoja.
-Nikaosha limao, naku kata na nilitumia kipande 1 kukamua maji ya limao, nika weka pembeni.

Jinsi ya kupika
1.Nika washa jiko.na kuinjika sufuria jikoni, kwenye kuku nika tia chumvi, limao, garlic Ginger Paste, manjano na mafuta. Kisha funika na mfuniko. Ni kaachha kuku achemke hadi maji yakauke.

  1. Nika ondoa mfuniko, hapa Sasa kwenye kuku yaka Baki mafuta tu, ambayo Ndio nikatumia kumkaanga kuku (shallow frying) hadi alipo vipande vyote vilipo badilika na kupata rangi ya brown.


3. Nikaweka kitunguu, nacho nikakikaanga hadi kikawa brown. Kisha nikaweka nyanya na kumix vizuri na mwiko. Nyanya na kuku, Kisha nikafunika na mfuniko, na kuacha nyanya viize hadi kulainika kabisa.

.
4.Nikachukua nyanya ya pakti na kuweka kwenye bakuli, nikatia maji kiasi na kukoroga vizuri. Kisha nikamimina kwenye kuku na kumix vizuri. Nikapunguza moto kidogo na kuacha mboga iendelee kuchemka kwa kwa dakika kadhaa. Nikazima jiko na kuku wangu wachuzi akawa tayari kuliwa.

Sisi tulimla kwa wali, kisamvu cha karanga na ndizi mbivu. Wewe ungemla na Nini? Share kwenye comments ❤️
.
Check pia recipe ya Kuku wa pilipli ( ni nzuri sana) bonyeza link hapa👇;
https://malkiawajiko.food.blog/2022/09/29/__trashed/

Design a site like this with WordPress.com
Get started