JINSI YA KUPIKA ORANGE-RED CHICKEN

Orange red chicken: hii niliandaa weekend, kwa ajili ya lunch. Tulikula na ugali na kachumbari.

-Mapishi yake ni rahisi sana, baada ya kumuosha kuku na kumkatakata, nikamwekea;
-chumvi kidogo sn
-limao kjiko 1 kikubwa
-garlic ginger paste
-orange red powder kijiko 1 kikubwa.

Kisha nikamix vizuri, na mikono kuhakikisha kuku kakolea viungo. Halafu Nika chukua grill pan, na kuiwekea mafuta kidogo, Kisha nikaweka vipande vya kuku kwenye grill pan na kuiweka kwenye oven.

Nika set moto 150 degrees na kuoka kwa dk kama hamsini, kuku akawa tayari kama unavyo ona. Ila ukipenda unaweza mkaanga.

-Kuku akatoka mtamu sana, tulifaidi ugali. Wewe huyu kuku ungemla na nini?

share kwenye comments pia usisahau ku-subscribe #malkiawajikoblog.

Design a site like this with WordPress.com
Get started