-Baada ya nyama kitu kingine nacho kipenda ni samaki, awe maji baridi au chumvi. Apikwe vyovyote vile mi nakula.❤️

-Hapa niliandaa vipande vya sangara . Baada ya kuosha vipande vya sangara i ni kakata vipande vidogo dogo, Kisha nikaacha vichuje maji.

Baada ya hapo, nikaanza kuweka viungo kama unavyo ona kwenye picha ;
-nimeweka curry powder kjk kikubwa 1
-pilau masala kjk kikubwa 1
-chumvi kjk kidogo 1
-garlic ginger paste kijiko 1 kikubwa
-limao kubwa 1

Kisha nikamix vizuri sana kwa kutumia mikono. Samaki na viungo vichanganyike vizuri. Halafu nikaweka samaki kwenye fridge kwa nusu saa viungo vikolee .

Baada ya hapo nikatoa na kukaanga kwenye mafuta kwa moto wa wastani, moto usiwe mkali sana. Samaki akatoka kakolee viungo, taste ni 🔥🔥 na ladha nzuri sana. Sangara wetu tulimla na ugali na kisamvu Cha nazi. #karibuni.

Wewe ungekula na Nini?? Share kwenye comments ❤️❤️❤️
Pia usisahau ku-subscribe, #malkiawajiko na kushare recipes zangu na uwapendao,thanks 🙏🏾