JINSI YA KUSAFISHA FRRIDGE (JOKOFU)

➡️Hello, leo napenda kushare kitu muhimu hasa kuhusu usafi jikoni, usafi wa fridge ⤵️
.
➡️ Usafi wa fridge ni kitu cha kuzingatia sana nyumbani kwako kwa afya ya familia yako kwani ni sehemu moja wapo unayotunza chakula (kibichi na kilichopikwa) cha familia. Lazima kusafisha fridge lako kila siku kila wiki usafi wa kawaida na kila mwezi usafi mkubwa. Yani usafi wa fridge mzima ndani na nje, na kuosha drawers na shelves za fridge. Ila kwa kila siku unatakiwa ukiona sehemu imechafuka kwenye fridge unafuta na kukagua vyakula ambavyo havifai na kuvitoa. Unapotaka kuanza usafi wa fridge zingatia vitu vifuatavyo.
.
➡️ Chomoa  wire wa fridge lako ukutani kutoka kwenye umeme (unplug),kuzuia shoti isitokee ukianza kusafisha.
.
➡️ Toa vyakula na vitu vyote kwenye fridge weka mezani, na kagua kama kuna ambavyo havifai tupa.
.
➡️Toa nje ya fridge drawers na shelves weka kwenye sink kisha osha na ziache zikauke au ukaushe kwa kitambaa.
.
➡️Weka maji kwenye bakuli chukua na kitambaa unachovya ndani ya maji ya motokad mua kisha safisha fridge kwa ndani ya fridge sio lazima utumie sabuni unaweza ongeza baking powder ni nzuri ktk kusafisha fridge.
.
➡️ Ukimaliza hapo safisha pia fridge yako kwa nje kwenye milango, kwa vile fridge kwa nje inachafuka sana unaweza kutumia sabuni kidogo, au dawa ya meno kusafishia kama kuna madoa doa itatoa kwa haraka.
.
➡️Baada ya hapo, rudisha drawers na shelves kwenye fridge yako, na anza kupanga vyakula vyako. Chomeka  tena wire wa fridge ukutani kwenye umeme. Basi kazi ya kusafisha fridge itakuwa imeisha.
.
Sijui wenzangu huwa mnafanya vipi usafi wa fridge? Comment yako muhimu tubadilishane maarifa.

Pia subscribe #malkiawajikoblog na follow account yange Instagram na Facebook ujifunze zaidi.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
📷: cleanmama

Design a site like this with WordPress.com
Get started