Leo napenda kuongelea kitu muhimu na kizuri sana chai masala au tea masala.
Wengi najua mnajua tea masala ni nini? Ila Kwa faida, tea masala tunaweza sema ni chai ya maziwa ambayo huwekwa majani ya chai na viungo.
☕️

Mimi viungo navyopenda kuweka ni iliki, mchaichai ulio kaushwa, mdalasini naongeza na majani ya chai meusi kisha naweka maziwa na kuchemsha hadi yatakapo kuwa tayari nachuja na kuinywa chai Yangu.
Tea masala ni chai nzuri sana, inaburudisha na spices zinafanya maziwa yawe na harufu nzuri, ladha tamu na inavutia kuinywa.
☕️

Tea masala unaweza kuweka viungo vingi zaidi ya hivyo, kwa mfano tangawizi ya unga, pilipili manga, karafuu nk.
Ila mi hizi spices 3 ndio naona combination yake inaendana vizuri ( iliki, mdalasini na mchaichai ulio kaushwa).
➡️jinsi ninavyo andaa viungo na kupika:
Huwa nachukua viungo vyote vile vizima navipasha moto ktk sufuria, hadi vianze kunukia nazima jiko, naviweka ktk kinu navitagwa hadi vilainike kisha nachekecha kutumia chujio, kupata spice podwer ile laini makapi siyatumii.
Wakati wa kupika chai naweka maziwa ktk sufuria, naweka majani ya chai ya African pride yale meusi, naweka na viungo vyangu vya tea masala nabandika sufuria jikoni, nachemsha maziwa kwa moto wa taratibu. Yakisha chemka vizuri hadi maziwa yaanze kubadikila rangi kama unavyo ona kwenye picha, nachuja chai yangu na inakuwa tayari kwa kunywa.
Je wewe unapikaje chai masala na unaweka viungo gani???? Share kwenye comments, 🙏

Usisahau kususcribe, like na ku share asante na endelea kujifunza mengi ktk blog yetu ya faida ya malkia wa jiko.