JINSI YA KUPIKA KUKU WA PILIPILI (#chickenpilipili)

Dinner menu; chicken pilipili, fries, salad and rosella juice

➡️Chicken Pilipili; huyu ni kuku wa kukaanga aliye tiwa pilipili na viungo vingine. Kama nilivyo sema kwenye post iliyo pita. Leo nita post, recipe ya #chickenpilipili. So ndio hii hapa,
➡️Mahitaji,

kuku wa kisasa 1(kl 1)
-pilipili mwendokasi 3
-pilipili mbuzi nyekundu3
-pilipili manga kjk 1 kikubwa
-binzari nyembamba1 kjk kikubwa
-kitunguu saumu 1,(toa maganda)
-tangawizi ya wastani (imenye)
-limao nusu
-chumvi kjk kdg 1
➡️Nilivyo tayarisha

  1. Baada ya kumwosha kuku, nika mkatakata vipande vya wastani. Na kumwacha pembeni achuje maji.
  2. Kisha nikachukua viungo vyote, nakuweka ktk kinu (kasoro limao na chumvi). Nika twanga hadi vika lainika.
  3. Nikachukua viungo na kuweka kwenye kuku, nikatia chumvi na kukamulia limao. Kisha nika mix vizuri kabisa ili viungo vienee ktk kila kila kipande cha kuku.
  4. Nikaacha kama nusu saa viungo vikolee ktk kuku, kisha ndio nika kaanga ktk mafuta, hadi kuku akawa brown. Nika toa nyama jikoni na ikawa tyr kuliwa.
  5. Hiyo ndio simple recipe ya kuku wa pilipili, ni mtamu sana anafaa kuliwa na chipsi, ndizi choma, pilau, ugali nk.
    ➡️Pilipili unaweza kuongeza au kupunguza, utakavyo penda.

➡️Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.

Design a site like this with WordPress.com
Get started