Hivi huwa unakuwa na ratiba ya vitafunwa vyako vya chai ya wiki nzima, au ndio yale mambo ya Giza likiingia ndio unaanza kukurupuka asubuhi chai inakuwaje??
. Napenda kuwa na ratiba ya kuniongoza kwenye mapishi, ili organised na kuokoa muda, maana unajipa ha mapema sababu unajua vitu gani ununue na utapika nini.
.
Ok
Karibuni maandazi; haya yanaenda na kinjwaji chochote kile utakacho penda. Moto au baridi.
Recipe yetu hii hapa;

Maandazi recipe
Mahitaji Ngano 400 gramu Mafuta 1/2 lita Sukari 100 gramu Maji 350 m/lita Hamira vijiko 2 vidogo
Jinsi ya kutengeneza
Weka maji kwenye bakuli yawe ya uvuguvugu kisha tia hamira koroga mpaka iyeyuke, kisha tia unga wa ngano katika bakuli kubwa ya kukandia, kisha tia sukari na mafuta kama vijiko vinne vikubwa katika unga, kisha tia maji uliyochanganya na hamira, anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika vizuri utengeneze donge moja kubwa.
Kisha baada ya kukanda acha kama dakika kumi na tano ngano yako, baada ya hapo ndio usukume na kukata shepu za maandazi unazotaka, acha yaumuke kama masaa mawili kisha kaanga. Unaweza kunywea chai maandazi au kinywaji chochote upendacho.
.
.
.
.
#maandazi #swahilifood #swahilicuisine #jifunzemapishi #simplecooking #jifunzemapishi #malkiawajiko #quickandeasyfood #tanzanianfood #tanzanianblogger #homecookfood #easyrecipes #simplerecipe #myrecipes