Mayai mvurugo, haya nilipika Jana kwa ajili ya breakfast. Nikaweka na kitunguu, hoho na karoti. Ni mazuri sana Kwa chai na fasta kutengeneza, recipe hii hapa;

Mahitaji
Mayai 6
Hoho 1 ya wastani
Karoti 1 ya wastani
Kitunguu kimoja kikubwa
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Sun flower oil vijiko 4 vikubwa
Jinsi ya kutengeneza
Baada ya kuosha hoho, karoti na kitunguu katakata vipande vidogo, vunja mayai, Tia chumvi na yapige pige na uma mpaka yachanga nyike vizuri.
.
Weka frying pan jikoni, Tia mafuta yakipata moto tia kitunguu viacha kama dk 1 viive, tia hoho na karoti kisha vigeuza geuza na uache navyo kidogo vichanganyike Vizuri, Kisha Tia mayai kwenye frying pan. .
Mara tu ukiweka mayai kwenye frying pan pale pale anza kuya vuruga vuruga na mwiko huku unahakikisha kila kitu kinachanganyika Vizuri, hadi utakapoona mayai yameiva na kubadilika rangi kuwa ya njano, zima jiko na yatoe weka kwenye sahani kwa kuliwa.
.
.
#malkiawajiko #mapishi#jikoni #jifunzemapishi #jiko #chakula #swahilifood #tanzanianfood #tanzanianblogger #mayai #friedeggs #breakfastrecipes #friedeggs🍳 #simplerecipe #cookinghome #easymealprep #easymeal #yummyfood😋 #quickrecipe #eggsforbreakfast #homecookingrocks #scrambledeggs