JINSI YA KUTENGENEZA CORN DOGS

Corn dog ni nini?? Ni kitafunwa, ambacho ni sausage iliyo wekwa kwenye kijiti na kuchovya kwenye mchanganyiko wa (ngano, Corn flour, mayai, maxiwa na viungo) halafu ika kaangwa kwenye mafuta.

My girls wanapenda sana, hizi corn dogs hivyo huwa naandaa home mara kwa mara . Ni kitafunwa kizuri sana na kinafaa kwa kinywaji baridi au moto.

Recipe yk ni simple sana, kama unashindwa kuandaa vitafunwa vingine kama chapati, Sambusa , vitumbua nk. Basi ujifunze hii recipe ni rahisi na itakupa confidence.

Mahitaji
+Sausage 8 (zikate katikati upate vipisi 16)
-maziwa fresh glass 1
-mayai 2
-ngano 1 kibakuli
-corn flour 1 kibakuli
-baking powder kjk kidogo 1
-chumvi kjk kidogo 1
-curru powder kjk kikubwa 1
-iliki, mdalasini ulio sagwa kjk 1 kikubwa
-mafuta kupikia chupa 1
.


Jinsi ya kuandaa

  1. Nilianza kuchemsha sausage kwa dk 3, Kisha nika weka pembeni zipie
  2. Nikachukua bakuli kubwa na kuweka ngano, corn flour, baking powder, chumvi, curry powder, iliki, na mdalasini, mayai na maxiwa.
  3. Halafu Nika chukua whisker na kumix taratibu hadi kila kitu kichanganyike vizuri, na mchanganyiko wangu ukawa kama uji mzito.
  1. Nika umimina kwenye glass nyembamba na ndefu
    5.Baada ya sausages kupoa, nikachukua vijoti 8 vya mishikaki . Nikavikata katikati vikawa 16
  2. Nika chomeka sausages kwenye kila kijiti
  3. Nikachukua sausage moja moja na kuchovya kwenye mchanganyiko wangu, na kisha nika kaangaa.
  4. Nika kaanga kwenye mafuta (deep fry) kwa dk kama 3, dk 3 zinatosha kuiva.

-Baada ya kumalizia kukaanga Nika waandalia my girls, wakala na kuenjoy .

ukitaka kuona video ya recipe bonyeza hii link hapa👇🏿

Design a site like this with WordPress.com
Get started