➡️Nyama ya ng’ombe: Hii imewekwa viungo vikakolea vizuri na kukaangwa ktk mafuta machache. Imetoka laini na ladha yk ni nzuri sana.
-Kama hupendi nyama yenye mchuzi pia hupendi iliyo kaangwa kwenye mafuta (deep fry) basi hii ndio sahihi kwako. Soma recipe mwanzo mwisho🥰

➡️Baada ya kuosha nyama, nika katakata vipande vidogo kisha nikaweka kwenywe grill pan(ambayo ndio nimetumia kupikia) unaweza tumia frying pan au sufuria ya kawaida pia.

-Kisha nikaweka chumvi kidogo tu, nikaweka maji ya ndimu, nikaweka tangawizi kitunguu saumu, nikatia pia manjano, na curry powder. Kisha nika mix vizuri kwa kutumia mkono, na kuhakikisha viungo na nyama vime changanyika vizuri. Kisha nikaweka mafuta kijiko kimoja na nusu kikubwa.

.
➡️Baada ya hapo nikaacha nyama iendelee kukolea viungo kama nusu saa hivi. Kisha nika weka grill pan jikoni. Baada ya kupata moto. Nyama ikaanza kuchemka, nikaacha ichemke hadi maji yakaukie kabisa. Kisha nikapunguza moto na kuaacha nyama iendelee kujikaanga na mafuta taratibu, huku naigeuza geuza na mwiko kila baada ya dk kadhaa.

Hadi ilipo kuwa tayari nikazima jiko na kuitoa jikoni. Hii inafaa kuliwa na ugali, pilau bubu, ndizi mzuzu, chipsi au kuitafuna yenyewe ukiwa na kinywaji chako pendwa pembeni. #karibuni

➡️Endelea kutembelea blog ya malkia wa jiko kujifunza mapishi zaidi na dondoo za jikoni. Pia subscribe, comment, lika na share na uwapendao.