JINSI YA KUTENGENEZA FRENCH TOAST

Hi, leo napenda kushare kitafunwa ambacho huwa napenda kula asubuhi mara kwa mara #frenchtoast . Hizi ni slices Za mkate zilizo chovya kwenye mayai kisha unazikaanga , mi napenda kuzipika sababu ni kitafunwa unachoweza kutengeneza Kwa haraka. Pia nikiwa sijisikii kula kitu kizito kwa lunch au dinnner huwa natengeza hizi #eggfrenchtoast  na inakuwa ndio mlo wangu. Na hivi ndio jinsi ya kutengeneza,

Vunja mayai 4 weka kwenye bakuli pana, unatia chumvi na iliki kijiko kidogo cha chai robo kisha unayapiga piga na uma mpaka yachanganyike. Unachukia mkate( slices 4 nimetumia, wastani slice moja yai 1) unazamisha kwenye mayai pande zote mbili kisha unakaanga na mafuta kiasi kwenye frying pan pande zote mbili uzikaange ziive hapo egg french toast yako itakuwa tayari, nimenywea na kahawa.

Karibu ku suscribe blog ya malkia wa jiko, ku like na ku comment thanks.

Design a site like this with WordPress.com
Get started