Kitchen tip: dondoo kuhusu glass, Inapendeza kuweka maji au vinywaji katika glass nzuri, safi na za kuvutia kwa ajili ya familia yako, wageni au zile siku maalum sherehe, sikukuu nk. Hapa kuna vitu vichache vya kuzingatia;
1. Ni vizuri kuwa na glass za kutosha kutumia watu wote pale inapohitajika, walau kuwa na seti 2 za zenye glass 12 kila moja.

2. Nunua glass za matumizi ya kila siku kwa ajili ya maji na vinywaji vingine hizi hata sisipo fanana zote sio mbaya maana kwa matumizi ya kila siku nyingine zinaweza kuvunjika ukitaka kununua za kuongezea usipate tena kama ulizo nazo.

3. Pia nunua glass kwa ajili ya matumizi maalum kama ukiwa na wageni au sherehe ni vizuri ikiwa set glass zote zinafanana, sababu unatumia kwa siku maalum ni rahisi kuzifatilia mwenyewe kwa ukaribu, kuliko kumwachia mtu mwingine.

4. Osha glass mara tu baada ya kuzitumia na usichanganye glass na vyombo vingine vilivyotumika hasa zinaweza kupata shombo, mafuta au kuweka mawingu mawingu ikasumbua kuosha.
5.Ukiosha glass usiweke sabuni nyingi zitateleza na kuvunjika kirahisi, pia zisuuze kwa maji ya kutosha na zikaushe au weka mahali zichuje maji.

6. Glass kama hujazitumia muda mrefu ukitaka kuzitumia ni vizuri kuziosha kwanza. Ukitaka glass zingae tia baking powder kijiko kimoja kikubwa au kamulia ndimu nusu kwenye maji utakayo tumia kusuuzia glass.
Asante kwa kutembelea blog ya malkia wa jiko karibu sana ujifunze zaidi kuhusu mapishi na dondoo za jikoni, pia subscribe, like, share na comment Ubarikiwe.