JIFUNZE AINA TATU MUHIMU ZA MDALASINI NA MATUMIZI YAKE

Ngoja niwape dondoo kuhusu mdalasini . Mdalasini, ni kiungo kimojwapo nakitumia mara kwa mara ktk mapishi. Iwe pilau, chai, supu nk. Hapa napenda ni share uzoefu wangu kidogo; Kama unaenda sn kwenye masoko makubwa km kariakoo, utakuta wanauza aina 3 za mdalasini (wanapima kwa kl), kuna wa Morogoro, India na Tanga. Kila aina ni nzuri na ladha na harufu iko tofauti, pamoja na muonekano wa nje.

  1. Mdalasini wa Morogoro, magamba yk ni madogo na haina harufu kali sn, mi huwa napenda kutumia hasa kwa chai na supu.

2.Mdalasini wa India magamba yake ni makubwa, harufu yk ni kali sn, iko juu sn na rangi yk inavutia na bei iko juu zaidi. Ila mimi sipendi kuutumia kwa mapishi. Ila natumia km manukato, kwenye mapishi harufu yk imenishinda hata kwenye pilau nikiweka nahisi kama nimepulizia perfume. So huwa nautumia kama air freshener jikoni, ukiuchoma au kuchemshesha jikoni pamoja na maganda ya limao harufu yake huwa nzuri sn. Hata kama nimeunguza chakula, huwa nafanya hivyo kuondoa harufu mbaya ya vyakula vilivyo ungua jikoni.

3.Mdalasini wa Tanga, ndio my favourite naupenda maana harufu yk ime-balance ni kali na nzuri, ila sio kali sn kupitiliza km ya India. Kwa pilau utapenda yani pilau linanukia kichakula chakula sio kama umeweka marashi kwenye chakula. Hataukimix na iliki ukasaga na kuweka kwenye maandazi au vitumbua yani taste inakuwa nzuri sana. Huu ndio huwa nanunua mwingi sababu kwangu unafaa kwa matumizi mengi.

Karibu kwenye comments ushare uzoefu wako au chochote kile kuhusu mdalasini.

http://malkiawajiko.food.blog

Design a site like this with WordPress.com
Get started