Leo napenda kuwapa kitu kizuri sana, hasa mnaopenda kupika kwa kutumia viungo, kama. Mimi #spicelovers.
Hapa nashare jinsi ya kuandaa #chickenmasala.

Hii masala Mimi huwa naandaa mwenyewe nyumbani, wala sio ngumu.
Huwa namtumia viungo hivi nane;
-tangawizi ya unga
-Vitunguu saumu vya unga (vilivyo kaushwa na kusagwa tyr)
-binzari manjano
-iliki
-mdalasini
-giligilani (mbegu)
-karafuu
-binzari nyembamba
.
Hivi viungo nane hapo juu, unaweza tengeneza chicken masala nzuri sana yenye viwango vya kimataifa. Ambavyo unaweza kutumia ku-marinate kuku atakaye pikwa vyovyote vile awe wa kukaanga, mchemsho, Choma, makange, chicken changamoto nk.
.

Mahitaji
Tangawizi ya unga
-vitunguu saumu vya unga
-binzari manjano
-iliki
-mdalasini
-giligilani (mbegu)
-karafuu
-binzari nyembamba
.

Vipimo kwa kila viungo vinatakiwa viwe Sawa, mifano mi huwa naweka vijiko 4 vikubwa vya chakula KWA kila viungo.
Ukitumia kipimo chochote kilingane KWA kile viungo.
Note; unaweza nunua viungo vilivyo sagwa tyr ukaja kumix mwenyewe nyumbani.
Au ukafanya kama Mimi navyo fanya, viungo navyo nunua tyr vimesagwa ni binzari Manjano, tangawizi ya unga, na vitunguuu saumu vya unga
Vilivyo baki nanunua vikavu nasaga mwenyewe nyumbani.
.

Jinsi ya kuandaa chicken masala
Niliweka frying pan jikoni, ilipo pata moto nikaweka mdalasini, iliki, giligilani, karafuu na binzari nyembamba nikaacha kama dk 3 vipate moto, utasikia vina anza kunukia, halafu Nika vigeuza geuza geuza na mwiko km dk 2. Nikazima jiko na kuviweka pembeni vipoe.
(Hivi viungo vyote niliweka kwa uwiano sawa vijiko 4 vikubwa)
.

Baada ya viungo kupoa , nikaweka kwenye kinu na kuvitwanga hadi vilipo lainika na kuwa unga, Nika vichekecha kutumia chujio , ili kuondoa makapi.
Kisha nikaweka kwenye bakuli, nika ongeza vijiko 4 vikubwa vya binzari manjano, vijiko 4 vikubwa vya tangawizi ya unga, vijiko 4 vikubwa vya vitunguuu saumu vya unga na kumix vizuri. Hapo Chicken Masala yangu ikawa tayari .
.
Unatakiwa kuhifadhi kwenye container Safi na Kavu, na kuweka mahali Safi, Salama, kusiwe na joto. Viungo vitakaa hadi miezi 6.
.

Unaweza Soma pia
https://malkiawajiko.food.blog/2023/09/20/jinsi-ya-kuweka-viungo-kwenye-samaki-fish-marination/
.
Usisahau ku like, comment, subscribe ili ujifunze Zaidi USIPITWE kila niki share post mpya. Pia share na uwapendao wajifunze Zaidi.