-Salad AFYA: hii salad ni tamu sana, yani kama una mtoto au hata mtu mzima hapendi mboga za majani, hii salad ndio solution yake.
Niliamua kupipa hilo jina, sababu hii salad ina mboga mboga mchanganyiko ambazo zote zina virutubisho muhimu kwa AFYA ya mwili.
.

Kama unavyo ona kwenye video, nimeweka nyanya, kitunguu, boho, Karoti, limao na chumvi, huwa naweka na Tango (ingawa hapa sikuweka)
Kuandaa hii salad ni rahisi, nikisha osha kila kitu, nakatakata vyote naweka kwenye bakuli, naweka limao na chumvi, namix vizuri na salad inakuwa tayari kuliwa.
.
Huwa kwangu tuna Kula na pilau, nyama choma, Ndizi choma, chipsi na chochote kile mtu atakavyo jisikia, au kula salad yenyewe tupu.
.

Tengeneza hii salad utakuja nishukuru, endelea kutembelea mallkia wa jiko blog utapa recipes nzuri sana na dondoo za jikoni.
.
-subscribe #malkiawajikoblog, ili usipitwe kila napo post
Pia like posts na share na uwaependao nao waongeze maarifa