FAHAMU VIUNGO VINAVYO PASWA KUWEKWA KWENYE SUPU

‎- Muulize Malkia wa Jiko: ‘viungo gani vinafaa kuwekwa kwenye supu’?
‎Hili swali huwa naulizwa na wengi mara kwa mara, nimeona nilijibu hapa kibarazani pia ili wengi mjifunze.

Supu ni chakula kinacho pendeza kiliwe kikiwa ktk uhalisia wake. iwe supu ya kuku, samaki au nyama aina yoyote Ile.
‎Namaanisha kwamba mapishi ya supu, yana takiwa kuwa simple,bila kuweka viungo vingi sana, hadi ladha halisi nyama iliyo kwenye supu ikapotea au supu ikabadilika rangi sana.

Mimi viungo navyo weka kwenye supu, ni hivi hapa ambavyo Ndio viungo msingi;
‎-tangawizi
‎-kitunguu saumu
‎-limao
‎-pilipili
‎-ndimu
‎Hivi viungo vinatosha kabisa kuifanya supu iwe na ladha nzuri na ya kuvutia, na walaji supu waka enjoy.
‎Viungo unavyo weza kuongeza , kwa wale wanao penda supu iwe hot and spicy, una ongeza pilipili manga na karafuu kidogo tu.
‎Pia kwa kuku wa kienyeji unaweka binzari manjano kidogo tu, ukitaka supu iwe na muonekano wa kuvutia.

KituKitu muhimu ili supu iwe tamu tumia kuku wa kienyeji, awe tetea au jogoo
‎ambao hawaja komaa sana
‎ samaki na nyama zinatakiwa ziwe fresh, zisiwe zimekaa sana kwenye fridge .
‎ .
‎Hizi dondoo ukizifatilia zita kusaidia sana, kwenye mapishi ya supu.
Search kwenye Malkia wa jiko blog post za mapishi mbalimbali ya #supu uongeze ujuzi jikoni.
‎.
‎subscribe, comment na share na wengine wajifinze

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started