- Matunzo ya miguu, Leo kwenye kipengele chetu cha #UREMBOJIKONI. Tunajifunza Jinsi ya kutunza miguu, kwa kutumia ingredients zinazo patikana jikoni kwako.
- Maana miguu ni kiungo kinacho fanya kazi kila wakati, kutembea hapa na pale. Kinapigwa vumbi, jua, baridi nk.
Hivyo usipo itunza inakuwa mikavu, migumu na yenye mipasuko

.
- Matunzo ya miguu, fanya kama ifuatavyo;
- Mara 2 kwa wiki;
Pasha maji moto hadi yawe ya uvuguvugu km Lita 3, halafu yaweke kwenye beseni.
Kamulia ndimu kwenye maji , weka na chumvi ya mawe kijiko 1 kikubwa. Mix vizuri, Kisha weka miguu yako kwenye beseni, hakikisha miguu(feet) imezama vizuri kwenye maji, na iloweke kwa dk 15 hadi 20..
Kuloweka miguu kwenye maji ya chumvi na ndimu, inasaidia ngozi ya nyayo za miguu kulainika haraka, hivyo ukija kusugua Gaga dead skins inatoka kwa urahiai. Pia kuondoa harufu kwenye miguu , na vilevile kutengeneza mazingira yasiyo RAFIKI kwa bacteria kuishi kwenye miguu yako.

Baada ya hapo kuloweka miguu, kifuatacho ni kusugua Gaga, hapa kazi inakuwa rahisi sana sababu, nyayo zinakuwa ziko laini. Tumia jiwe laini kusugua Gaga au foot file. Unasugua Gaga taratibu hadi uone dead skins zimetoka zote. Kisha kunguta miguu vizuri, inawishe na maji, halafu ikaushe vizuri kabisa.

Kinacho fuata paka mafuta, lotion au cream kutegemea na wewe unacho tumia. Ukimaliza kaa pumzika iache miguu ipate hewa kabla ya kuendelea na mambo mengine
.
Note: kama una fungus miguuni hakikisha umepata dawa kutoka kwa daktari utumie hadi upone, ndio uje kuendelea na mambo haya.

.
- Matunzo ya miguu kila siku
Ili kuepusha miguu kuwa mikavu na kupasuka. Hakikisha;
-hutembea peku kwa muda mrefu hata ukiwa ndani ya nyumba vaa viatu laini kwa ajili ya ndani.
-kuepuka miguu kupigwa baridi vaa soksi na hakikisha miguu unapaka mafuta.
-Osha miguu kila mara inapokuwa na vumbi
-miguu yenye mipasuko kila jioni osha vizuri, ikaushe na paka mafuta ya Nazi, Kisha uwe unavaa na kulala na soksi usiku. Inasaidia miguu kuwa laini na kutibu mipasuko.
-ukiwa unafanya sana kazi za nje, mfano shambani hakikisha kila ukimaliza kazi unaosha miguu yako na kujisugua kwenye jiwe. Itakusaidia miguu isipate mipasuko na magaga .

Hivyo ndivyo unavyoweza kutunza miguu yako, kwa njia rahisi kabisa nyumbani kwako, bila gharama kubwa. Karibu ushare kwenye comments njia nyingine ambazo unatumia kutunza miguu yako.❤️
Pia kumbuka ku-subscribe #malkiawajikoblog , like na kushare post hii na uwapendao wajifunze pia.
