JINSI YA KUWEKA VIUNGO KWENYE [ nyama, samaki na kuku]- UTANGULIZI

Mboga au kitoweo, hasa chenye asili ya protini mfano nyama, samaki na kuku. Kinakuwa na ladha nzuri unapo weka viungo vya chakula, unapo pika iwe kwa kukaanga, kuchemsha au kuchoma.

Kazi za viungo kwenye hizi mboga ni; kuongeza ladha, kulainisha nyama, kufanya mboga iwe na rangi ya kuvutia na inukie. Viungo vya chakula mimi nimeviweka kwenye makundi mawili, nayo ni moja viungo msingi na pili viungo sekondari.

Viungo msingi; hivi ni viungo ambavyo mimi lazima niweke kwenye mboga yoyote nikipika. Navyo ni tangawizi, kitunguu saumu,limao, pilipili na chumvi.Mimi nikiweka viungo hivi, sio lazima niongeze viungo vingine kwenye mboga. Hivi viungo vinatosha kabisa kuifanya mboga iwe na ladha, inukie na haitapoteza uhalisia wake. Hivyo kama haupendi kuweka viungo vingi kwenye mboga zako, hivi viungo pekee vina tosha kabisa. Na post zijazo nitakuelekeza na kushare recipes za samaki, kuku na nyama ambazo nimetumia viungo msingi tu. #usikaembali

Viungo vya ziada; hivi ni viungo huwa naongeza kwenye mboga baada ya kuweka viungo vya msingi. Hapa viko viungo vingi sana, maana ni viungo vyote isipo kuwa viungo msingi nilivyo taja hapo juu. Kutaja vichache manjano, curry powder, giligilani, soy sauce, paprika, mdalasini, kungumanga, mustard,garam masala nk. Hivi viungo ukiweka kwenye mboga, lazima itabadilika kuanzia rangi, harufu itabadilika maana viungo vitanukia sana kuipita harufu original ya mboga, hata ladha pia ita change. Yani kama ni nyama ukila utapa taste ya nyama ikiwa imemix na viungo [ ladha inakuwa 50/50], tofauti na viungo msingi, ladha ya nyama inabaki kwenye uhalisia wake ladha ya viungo ipo ila kwa mbali, haiwezi kuzidi au kuifunika ladha ya nyama.

Hapa nakupa maelezo ya utangulizi na muhimu sana uelewe na elimu hii itakusaidia sana ukiwa unapika nyumbani, pia uweze kufanya uchaguzi sahihi wa viungo kulingana na nini unapenda. Hupendi viungo vingi basi utatumia viungo msingi na sie tunaopenda viungo vingi basi tuna uwanja mpana wa kuutumia na kuonyesha mbwembwe zetu kwenye mapishi. Kama nilivyo sema nitashare recipes nyingi tu ili ujifunze, na kuongeza ujuzi na hilo ndilo lengu langu la kuanzisha blog hii.

Hivyo usiache kufatilia somo hili ‘jinsi ya kuweka viungo kwenye nyama, samaki na kuku’ huu ni utangulizi recipes zinakuja hivyo subscribe usipitwe na chochote. Pia like, comment na share na uwapendao wajifunze pia. THANKS

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started