JINSI YA KUCHOMA MISHIKAKI YA NG’OMBE (FOR BEGGINERS)

Leo napenda nikupe ujanja kidogo, kama Bado hujawa konkii master kwenye kuchoma mishikaki.

Nakuelekeza njia simple kabisa na mishikaki itatoka vizuri sana;
-ikiwa imeiva hadi ndani,
-Imekolea viungo,
-taste nzuri,
-laini
-imeiva bila kuungua

Kama unafatilia post zangu utagundua nyama Choma ni kitu ninacho kipenda. Na jumamosi niliandaa mishikaki kwa ajili ya lunch.
Maana kwangu weekend napenda iwe ni #foodfamilyfun

Hapa nilitumia nyama steak, nusu kilo (ilikuwa na mafuta kiasi sio sana). Na viungo niliweka curry powder (Simba mbili), kitunguu saumu, tangawizi, limao na chumvi.

Baada ya kuosha nyama na kukatakata, nikaweka kwenye chujio na kuacha ichuje maji. Kisha nikaweka viungo na ku- mix vizuri, nili hakikisha kila kipande cha nyama kimepakwa viungo. Baada ya hapo nikaweka kwenye stick za mishikaki. Halafu nika acha nyama kwa dk30, viungo vikolee vizuri, kabla ya kuichoma.

-Baada ya hapo nikachukua #grillpan ( kama huna) tumia hata #fryingpan, Nika iweka jikoni ilipo pata moto, nikaweka mishikaki, nikawa naigeuza kila baada sekunde kadhaa, hadi nilipo ona nyama haitoi maji tena. (Hapa mishikaki inakuwa imeiva ila haijakauka)
Nikazima Jiko na kuihamishia mishikaki kwenye oven.

-Moto niliset 100 degree (kwa dk kama 15 au 20), kwenye oven mishikaki ikaendelea kuiva na kukauka taratibu. Kama huna oven tumia mkaa, ila moto usiwe mkali sana. Mishikaki itaiva vizuri sana bila pressure.

-Njia hii ni simple na nzuri sana, kama Bado Ndio unajifunza kuchoma nyama. Itakuwezesha utoe kitu Cha uhakika bila kuharibu.
.
–Ukihitaji dondoo 5, muhimu jinsi ya kuandaa nyama Choma, utazipata kwa TSH 1,500/= utajifunza vizuri uchaguzi wa nyama, jinsi ya kuweka viungo, na jinsi ya kuchoma. Wasiliana nami whatsap 0657 234 897.

Ok, karibu kwenye comments tunadilishane uzoefu kuhusu mishikaki/nyama Choma😍

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started