JINSI YA KUWEKA VIUNGO KWENYE SAMAKI (fish marination)

➡️Muulize Malkia wa Jiko: “MJ naomba nielekeze jinsi ya kuweka viungo kwenye samaki “
-Kama mjuavyo huwa napata maswali mengi na huwa najibu kutokana na nafasi yangu. Kama hili nimeona nishare hapa kwa faida ya wengi.


➡️Hapa nitaongelea jinsi ya kuweka viungo kwenye samaki awe wa maji chumvi au baridi. Ila ambaye atapikwa kwa njia ya kukaanga au kuchoma. Wa kuchemsha au supu uwekaji wa viungo ni tofauti kidogo, tutaongelea muda mwingine.

➡️Mimi samaki nikisha msafisha na kumkata kata. Huwa namwacha achuje maji yote. Kisha baada hapo ndio na mwekea viungo. Ambavyo ni curry powder, binzari manjano na binzari nyembamba, pia kitunguu saumu, tangawizi, limao, pilipili na nitaweka na chumvi.


➡️Natwanga kwenye kinu kwa pamoja tangawizi, saumu, binzari nyembamba na pilipli. Natwanga taratibu hadi vilainike kabisa, Kisha naweka binzari manjano na curry powder na mix vizuri viungo vyote kwa pamoja . Baada ya hapo ndio napaka viungo kwenye samaki. Kisha nakeka limao na chumvi.

Baada ya kuweka viungo samaki, naweka samaki kwenye fridge ili kutoa nafasi viungo vikolee vizuri. Kama nina haraka naweza kumuacha kwa nusu saa au saa moja. Ila Kama nina muda wa kutosha huwa namwacha kwa masaa mengi zaidi. Samaki akitoka hapo ananukia, na ukikaanga anatoka na Rangi nzuri na ladha tamu yani utaenjoy. Ila wakati wa kupika hakikisha moto usiwe mkali sn.

➡️Pia napenda kusikia kutoka kwako huwa unapikaje samaki na viungo gani unaweka???? Share kwenye comments tujifunze zaidi. 💚♥️.
-Usisahau ku-subscribe #malkiawajikoblog uendelee kujifunza mapishi bila kupitwa na post mpya.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

One thought on “JINSI YA KUWEKA VIUNGO KWENYE SAMAKI (fish marination)

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started