JINSI YA KUANDAA MISHIKAKI YA NGO’MBE [ ORANGE RED MISHIKAKI]

️Mishikaki ya Ngo’mbe (orange red mishikaki ): hii niliandaa kwa ajili ya kusherekea mwaka mpya. Ilikuwa mitamu sana, viungo vilikolea vizuri na nilimetumia steak, ambayo haikuwa na mafuta mengi.

➡️Nilitumia orange red powder kwa ajili ya kuipa mishikaki hiyo rangi mnayo iona, pia viungo niliweka vichache tu tangawizi, kitunguuu saumu na limao.

. ➡️Baada ya kuosha nyama na kukatakata vipande vya wastani, nikaweka, kitunguu saumu, tangawizi na limao.

Nika mix vizuri viungo na nyama, kisha nikaweka orange red powder(vijiko 3 vikubwa) .Hii orange red nili mix na maji kidogo tu. Kisha ndio nika weka kwenye nyama na kumix tena vizuri hadi nilipo ona viungo vime jimix vizuri na nyama.

Note: sikutia chumvi sbb hii food colour (orange red ina chumvi chumvi) na walaji wangu mi hawataki chumvi nyingi.

➡️Baada ya hapo nikaweka nyama kwenye vijiti vya mishikaki, kisha nikaweka mishikaki kwenye fridge kama saa nzima viungo vikolee zaidi.

➡️Baada ya hapo, mishikaki nilianza kwanza, kugrill kwenye (grill pan), kwa moto wa wastani hadi nili- poona nyama haitoi tena maji, yani inaanza kutoa mafuta baada ya kupata moto ndio nika hamishia kuendelea kuichoma kwenye oven 200°C, setting niliweka (grill) kwa dk 30 mishikaki yangu ikawa tayari. #karibuni .

➡️Subscribe #malkiawajikoblog kujifunza mapishi zaidi na kupata dondoo za jikoni, pia karibu kwenye comments kushare ulilo nalo, uisahau kuwakaribisha uwapendao nao wajifunze.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started