JINSI YA KUPIKA MBOGA YA BAMIA NA NYANYA CHUNGU

➡️➡️Mboga ya bamia na nyanya chungu. Hii nilipika jana mchana kwa lunch. ➡️Mimi napenda mboga za majani karibu zote tu. Hasa kula na ugali, na nyama choma.😍😍.

Hapa nilitumia zile nyanya chungu original (zile nyanya chungu halisi kabisa ndogo ndogo zenye uchungu wake) sio zile nyeupe tamu..So kuepuka mboga yote kuwa na uchungu uchungu, hizi nyanya chungu mimi huwa nazi chemsha na mvuke kwanza, halafu huwa nakuja kumix na bamia mwishoni kabisa. Bamia zikiwa zimeiva.

.➡️Recipe hii hapa;

Mahitaji

– Bamia robo kl

– Nyanya chungu 10 (unaweza kutumia pia zile nyeupe kubwa zisizo na uchungu ila unazipika pamoja bamia toka mwanzo]

– Kitunguu 1

-Nyanya maji 4 kubwa (saga kwenye blender weka maji kdg)

-Nyanya ya pakti vjk 2 vikubwa

-kitunguu saumu kjk 1kdg

-curry powder kjk 1

kdg-Binzari manjano kjk1

kgd-Pilipili -mafuta ya kupikia (jikadirie).

Jinsi ya kupika

➡️ Niliweka mafuta ktk sufuria na kuwasha jiko, yalipo pata moto, nikatia kitunguu nika kikaanga hadi kikawa brown. Nikaweka kitunguu saumu, nika mix vizuri na kitunguu maji kama sekunde 10. Kisha nikatia nyanya maji na nikafunika na mfuniko.

.➡️Nikaacha nyanya hadi zilainike kabisa, nikatia nyanya ya pakti, binzari manjano , curry powder, na chumvi. Kisha nikamix tena kwa kutumia mwiko kila kitu kichanganyike vizuri kabisa, halafu nikaweka bamia na pilipili.Nikaacha vichemke hadi mchuzi wa nyanya ulipoñanza kukaukia, nika geuza vizuri na mwiko kisha nikaweka nyanya chungu, nika acha mboga jikoni iendelee kuchemka kama dk mbili, nikazima jiko na kuweka sufuria pembeni.

.➡️ Hapo mboga yetu bamia na nyanya chungu likawa tayari, ikaliwa kwa ugali na nyama choma. Karibu kwenye comments ushare chochote kuhusu nyanya chungu.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

One thought on “JINSI YA KUPIKA MBOGA YA BAMIA NA NYANYA CHUNGU

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started