KUKU CHOMA ALIYETIWA CURRY POWDER

Kuku choma (grilled chicken curry) : hapa nime share kuku choma, ambaye ametiwa curry powder kama kiungo kikuu na vikolobwezo vingine. Recipe yetu hii hapa;


Mahitaji
-Kuku mzima ( msafishe na mkate kate) mi nimetumia Kuku 2 sababu wakikuwa na size ndogo.
-curry powder vijiko 4 vikubwa -tangawizi kijiko 1 kidogo
-kitunguu saumu vijiko 2 vikubwa
-limao 1 kubwa
-pilipili manga kijiko 1 kidogo
-chumvi kijiko 1 kikubwa

Matayarisho

Baatda ya kumsafisha Kuku, nika mkata kata ktk vipande vya wastani. Kisha nikamweka kwenye chujio achuje maji hadi yalipo isha kabisa.


Nikamtia curry powder, tangawizi, saumu, pilipili manga, limao na chumvi. Nikachanganya na kumpaka viungo vizuri nime hakikisha kila Kipande kimekolea viungo. Nilipo maliza nika mweka Kuku kwenye fridge Kwa nusu saa (viungo vikolee vizuri). –

Baada ya hapo nikamitoa Kuku na kumchoma kwenye oven Kwa moto wa taratibu.

🍗
Alipo iva akaliwa na ugali pamoja na mchicha. Ndio ilikuwa lunch.

#karibuni

🍗
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.
.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started