Jumamosi my girls walikuwa busy kupractice recipe Kwa ajili ya #christmasbiscuits, wanajua kutengeneza biscuits na #cookies, Ila walikuwa hawajawahi tengeneza special Kwa, hope wakisha practise Mara ya 2 na 3 ikifika #xmas wata bake best biscuits.

Hii ndio recipe yao;
Christmas #biscuits #recipe
Mahitaji;
-Ngano- robo kilo (250 gram)
-Sukari- vijiko 5 vya kulia chakula
-Siagi- vijiko 3 vya kulia chakula
-Mayai 2 makubwa
_baking powder kijiko 1 kikubwa
-sprinkles

Vifaa utakavyotumia;
-Rolling pin(ya kusukumia chapati)
-Mwiko
-Kibao cha kusukumia chapati / au kukatia vitu jikoniBiscuits cutter
-Bakuli kubwa (Mixing bowl)

Jinsi ya kutengeneza
1-Weka sukari kwenye bakuli
2- Halafu weka Siagi, kisha changanya Siagi na sukari kwa kutumia mwiko mpaka vichanganyike
Weka mayai na endelea kuchanganya na mwiko, Kisha weka ngano changanya vizuri kisha ukande kidogo
3 – Ukimaliza kukanda unga , gawanya Vitoke viduara vitatu, chukua kiduara kimoja kimoja weka katika kibao chako sukuma ( kama chapati) kisha chukua cams biscuits cutter kata maumbo unayo taka
4 – baada ya kukata weka biscuits kwenye baking tray na mwagia juu yk sprinkles kisha ziweke pembeni, wakati ukisubiri oven ipate moto.
5 – Washa oven yako, moto 150C/390F subiri zipite dakika tano, kisha weka biscuits.

Ziache ndani ya oven dakika kama 15, au kama unataka zikauke zaidi ziache dakika ishirini.
Baada ya hapo biscuits zitakuwa tayari, zitoe nje ya oven na ziache kidogo zipoe, baada ya hapo zitakuwa tayari kuliwa.