ROSEMARY CHICKEN CHOMA

➡️ rosemary kuku choma; Huyu kuku nimemwekea viungo ila majani ya rosemary ndio kiungo kikuu. Jana usiku baada ya kumsafisha kuku na kumkata kata, nilimkata vipande 5. Mapaja 2, vidari 2 na kipande ni shingo iliyo unganika na mgongo.


➡️Nikaweka vipande vya kuku ktk beseni nika kataka kata majani ya rosemary vipande vidogo vidogo na kuweka ktk kuku, nikaweka pia limao, tangawizi, kitunguu saumu na chumvi kidogo nika hakikisha viungo vyote nime vipaka vizuri ktk kuku, kisha nikaweka kuku ktk fridge usiku mzima aendelee kukolea viungo.

➡️Mchana nikamtoa na kumchoma ktk oven kwa moto wa tararibu, alipo karibia kuiva nikatoa kuku na kuipakaza ketchup kidogo kisha nika rudisha tena kwenye oven imalizia kuiva. Rosemary kuku choma tulimla kwa ugali na kachumbari ya pilipili.


➡️ Usisahau ku-like, comment na ku-share

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started