Hope mko poa, leo napenda kushare recipe muhimu ya kitu nacho kipenda sana, supu ya kuku wa kienyeji. Kama una fatilia post zangu vizuri utakuwa umegundua huwa napenda kupika mapishi ambayo ni simple na yasiyo tumia muda mwingi.

Kitu cha kwanza nacho zingatia kwenye maandalizi ya supu ya kuku wa kienyeji, ni kuchagua kuku ambaye bado kijana, wale ambao hawaja komaa sn na mara nyingi napendelea jogoo.

Baada ya kumwosha kuku na katakata vipande, namweka ktk sufuria kubwa, nitia chumvi kijiko 1 kidogo, limao kubwa 1, tangawizi na kitunguu saumu kisha nikaweka maji lita 2. Wakati mwingine naweka viazi mbatata nakata vipande vidogo dogo huwa vikiiva vinasaidia kufanya supu iwe nzito nzito.

Baada ya hapo nabandika jikoni, naacha ichemke hadi iive ikaribie kuiva. Kisha naweka karoti, hoho na mbogamboga nyingine kama zipo, naacha viendelee kuchemka hadi nyama iive kabisa kisha nazima jiko na hapo supu yangu ya kuku wa kienyeji inakuwa tayari kwenda mezani. Pilipili huwa naweka wakati wa kula sababu ya watoto siwezi weka moja kwa moja kwenye supu.

Supu ya Kuku wa kienyeji mi hupend kula na chapati, ndizi mzuzu choma, viazi mbatata vya kuoka au mkate.#karibuni
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.
