-Banana milkshake🍧🥛; ni kinywaji pendwa cha wanangu wanapenda kutengeneza hasa weekend. Ni kinywaji kizuri na rahisi kutengeneza.

Hapa walitumia ;
-ndizi 3
-maziwa fresh nusu lita (yawe baridi)
-ice cream (vikopo vidogo 3)
-vanilla flavour kijiko 1 kikubwa
-chocolate biscuits pakti 1

Weka kila kiti ktk blender, kasoro biscuits. Saga hadi mchanganyiko uwe laini, mimina ktk glass, vunjavunja biscuits na ziweke juu ya milkshake, weka mrija kwenye glass na banana milkshake yako itakuwa tayari kwa kunywa.
Note: unaweza kuweka au usiweke ice cream

Asante kwa kutembelea malkia wa jiko, karibu tena na usisahau ku-follow, like na kuacha comment. Kumbuka kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima. Milo yote 3 iko ktk soft copy, tsh 10,000 whatsaap 0752 741 831.