JINSI YA KUPIKA CHAPATI MAJI

Chapati maji ni kitafunwa kizuri sana na fasta kupika na kinasaidia kukupa fursa ya kubadilisha vitafunwa, sio kula mikate kila siku inachosha. Hapa nashare recipe yangu jinsi ya kupika chapati maji nzuri na tamu.
Recipe yangu ya chapati maji hii hapa.


Mahitaji –
ngano 300gramu,
maziwa glass 1 ndogo,
mayai 2,
sukari kiasi vijiko vikubwa 2,
maji glass 2,
Mafuta vijiko 5 vikubwa


. jinsi ya kutengeneza
Mi nilitumia mixer, kuchanganya kila kitu, ingawa Pia unaweza kutumia blender au hata Kwa mkono. Niliweka kila kitu ktk mixer kasoro mafuta. Baada ya mchanyiko wangu kuwa tayari nikaumina ktk bakuli, nikatia mafuta ktk mchanganyiko wangu, nikakoroga taratibu hadi mafuta yakachannyika vizuri.
Njia ya kuchanganya mafuta ndani ya tuite ule uji wa chapati naipenda maana wakati wa kupika huweki tena mafuta, unapika chapati kwenye kikaango Bila kuweka mafuta sababu uji wenyewe wa chapati una mafuta tayari, na inasaidia chapati zinatoka nzuri Bila kuwa na mafuta mengi.

Ok, tuendelee baada ya hapo nikaweka baada ya hapo nikaweka frying pan jikoni, ilipo pata moto nikachota mchanganyiko wangu upawa 1 na kumimina kwenye frying pan nika acha kidogo iiv e n a kugeuza upande wa pili ilipo iva nikatoa na kuendelea hivyo hadi zikaisha. πŸ‘‡πŸΏ
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.

Asante kwa kutembelea malkia wa jiko blog

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started