JINSI YA KUTENGENEZA MAYAI MVURUGO

Leo napenda kushare recipe ambayo ni simple kuhusu mayai ambayo huwa naweka vitunguu, hoho na karoti. Kutokana na jinsi navyo yapika mi hupenda kuyaita mayai mvurugo.

Mayai mvurugo ni mazuri sana kwa chai pia yanafaa kuliwa na kitafunwa chochote kile, na unaweza kula na ugali hata wali , recipe hii hapa;

Mahitaji-

Mayai 5, Hoho 1 ya wastani,Karoti 1 ya wastani ,Kitunguu kimoja kikubwa,Chumvi kijiko kimoja cha chai,Sun flower oil vijiko 4 vikubwa.

Jinsi ya kutengeneza

Baada ya kuosha hoho, karoti na kitunguu katakata vipande vidogo weka pembeni, vunja mayai weka kwenye bakuli, tia chumvi na yapige pige na uma mpaka yachanga nyike vizuri. Weka frying pan jikoni, tia mafuta yakipata moto tia kitunguu viacha kama , tia hoho na karoti kisha  vigeuza geuza vichanganyike vizuri, kisha tia mayai kwenye frying pan na mara tu ukiweoka mayai kwenye frying pan pale pale anza kuya vuruga vuruga na mwiko huku unahakikisha kila kitu kinachanganyika vizuri, hadi utakapoona mayai yameiva na kubadilika rangi kuwa ya njano, zima jiko na yatoe weka kwenye sahani kwa kuliwa.

Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.

Published by eunicemahundi

Hi🙋🏾, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: 📧 eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started