Jinsi ya kuweka viungo kwenye nyama ya Kuku; kama nilivyo sema post iliyo pita, nitaelekeza jinsi ya kuweka viungo kwenye kuku, hii inafaa kwa kuku choma au kuku wa kukaanga.
.

.
Kitu cha kwanza kukumbuka , ili kuku awe na ladha tamu, na nyama itoke ikiwa laini. Hii ndio kitu muhimu sana, ukisha weka viungo kwenye kuku unatakiwa kabla ya kuchoma au kukaanga nyama uiache, walau kwa saa 1 au hata masaa 4, au zaidi ili viungo vikolee vizuri hadi ndani. Ukiona kuku kawekwa viungo na bado hana ladha, sababu huwa kawekwa viungo muda huo huo Kisha akachomwa au kukaanga.
.
🍗 Osha kuku, kisha katakata vipande vya wastani( Kama itahitajika kufanya hivyo, visiwe vikubwa sana au vidogo sana) weka kwenye bakuli kisha tia chumvi, limao.
.

Chukua tangawizi, kitunguu saumu, binzari nyembamba, pilipili manga, mustard na pilipili mbuzi. (Tumia viungo ambavyo ni fresh) vichanganyike viungo vyote kwa pamoja, saga au vitwange kisha uweke kwenye nyama, hakikisha vizuri nyama umeipaka viungo vizuri.
.
🍗
Weka kuku katika fridge, kwa masaa kadhaa ukiwa na haraka at least nusu saa. Acha kuku akolee viungo taratibu, Kisha ndio uchome kwenye oven, mkaa, au electric grill, kwa moto wa taratibu ili atoke ameiva vizuri na laini.
.

Uki kaanga hivyo hivyo hakikisha moto sio mkali sana, na wakati wa kutia kuku kwenye mafuta hakikisha haya japata moto sana, maana nyama itaanza kuungua kwa nje na ndani haitaiva vizuri.
.
🍗
Ukifanya hivyo Kuku wako atatoka vizuri uta enjoy, Kama Ulikuwa Bado unafikiria kitu cha kupika kesho weekend, jaribu hii.
.
Napenda mapishi sana
LikeLike
karibu sn Jasmin
LikeLike
Yummy
LikeLike
Thanks dear 🙏🙏
LikeLike
Niceee
LikeLike
Thanks Rosee
LikeLike
naweza kutia viungo nikailaza ktk friji Usk nikapika kesho yake?
LikeLike
Ndio unaweza, na inakolea viungo vizuri ila usiweke chumvi na limao, hadi utakapo kuwa unakaribia kupika.
LikeLike
hongera mam huna darasa la kufundisha dia?
LikeLike
Thanks dear, kwa Sasa Sina darasa napost tu Instagram na hapa kwenye #malkiawajikoblog
LikeLike