Cupcakes : hizi wamepika girls jana, zimetoka vizuri na tamu, wameshajua kubake cupcakes makosa ni madogo tu. Kitu wanacho jifunza sasa hivj ni jinsi ya kupamba cupcakes.
.

Hizi ni simple kutengeneza mtoto wa grade 1 unaweza anza kumfundisha, na inakuwa rahisi zaidi ukitumia hand mixer au hand whisker ya umeme.
.
ππΏ
Simple Cupcake Recipe
Mahitaji (Kwa cupcakes 12)
-ngano 100 gram
-chocolate powder 50 gram ( nimetumia nesquick) unaweza tumia milo, cacao nk
-mayai makubwa 2
-baking powder kijiko 1 kidogo
-white sugar vijiko 3 vikubwa
-maziwa nusu kikombe(mug)
.
ππΏ
Utahitaji: cupcake baking tray na cupcake papers
.

Jinsi ya kuandaa
1. Washa Oven 160 – 180 degrees
2. Chukua bakuli kubwa, weka kwanza butter na sukar, mix vizuri kwa kutumia whisker ya umeme ( Kama huna tumia ya mkono, au mwiko mwembamba)
3. Vikisha changanyika vizuri, weka mayai endelee kumix hadi mchanganyiko uwe laini
4. Weka ngano, chocolate powder, baking powder na maziwa, endelea kumix hadi kila kitu kimechanganyika vizuri.
5. Zipange cupcakes paper kwenye baking tray, Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye cupcake papers.
6. Weka baking tray yako kwenye oven na oka Kwa dakika 20, cupcakes zitakuwa tayari.
7. Kama unajua ku decorate cupcakes unaweza endelea na hatua hii, ikiwa no vipi unaweza anza kuzila π.
ππΏ

Cupcakes, cookies, biscuits ni kitu rahisi vya kuanzia kuwafundisha Watoto kujifunza mapishi, mi wako likizo na hivyo wako busy na jiko, wana tengeneza wenyewe vitu wanavyo penda.

I like this
LikeLike
thanks
LikeLike