MKATE WA UFUTA RECIPE

Mkate wa ufuta; umeshawahi kula au kuupika??! ni mkate mzuri sana kwa chai, pia ni simple sn kuupika hauna usumbufu. .
Mimi napenda kuupika sababu inanisaidia kuweza kubadili vitafunio kwa ajili ya chai. .
β˜•οΈπŸ΄πŸ΄
Unaenda vizuri na tea masala, chai ya rangi, kahawa. Na unaweza kuongeza vitu vingine utakavyo penda wakati wa chai.

Mkate wa ufuta recipe
πŸ‘‡πŸΏ
Mahitaji
Ngano Robo kilo
Maji Vikombe 1(mug)
Sukari vijiko 4 vikubwa ( vya kulia chakula)
Hamira Vijiko 2 vidogo
Yai 1
Ufuta Vijiko 3 vikubwa
Mafuta Vijiko 7vikubwa .

Jinsi ya kutengeneza
Weka maji kwenye bakuli yawe ya uvuguvugu kisha tia hamira koroga mpaka iyeyuke (weka pembeni), kisha tia unga wa ngano katika bakuli kubwa ya kukandia, piga piga yai nalo liweke kwenye ngano, kisha tia sukari na mafuta vijiko vitamo vikubwa katika unga, kisha tia maji uliyochanganya na hamira, anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika vizuri na umekuwa laini, utengeneze donge moja kubwa. Liweke pembeni kama dakika 15.

Baada ya hapo sukuma donge la ngano lisukume utengeneze umbo la duara, kisha paka mafuta kijiko 1 upande wa juu na chini, na tayarisha chombo cha kuokea nacho paka mafuta kijiko 1, weka mkate uliosukuma ndani ya chombo cha kuokea, , kisha chukua ufuta mwagia juu ya mkate pia, kisha uweke pembeni mkate uumuke kama saa 1.

Baada ya hapo oka kwenye oven, weka moto 220 C ( namba 5), oka kwa dakika 20-30
.
Mpaka uone mkate umepata rangi ya brown, mkate wako utakuwa tayari. Mkate huu wa ufuta ni mzuri kwa chai, ili pia unafaa Kwa supu, mchuzi wa samaki au mchuzi wa nyama.
Hope utajjaribu kuupika uje hapa kutupa mrejeshoπŸ˜ƒ,
.
Kupata rariba ya chakula/mapishi ya mwezi mzima, milo yote 3 iko ktk soft copy Whatsap 0752 741 831.

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started