Omelette Burger 🍴, hii nimetengeneza leo mchana kwa ajili ya lunch ni nzuri sn girls wameipenda.

Mkate wa burger nilinunua super market, Kwa hiyo nili tengeneza omellete, nilitumia mayai 4, karoti 2, kitunguu 1 na hoho 1.
.
🍔
Nilivunja mayai na kuweka kwenye bakuli kubwa, Kisha nika katakata kitunguu, hoho na karoti vipande vidogo nikaweka pia ktk bakuli nililo weka mayai, nikatia chumvi kijiko 1 kidogo, kisha nika piga piga mayai Kwa kutumia uma hadi kila kitu kinachanganyika vizuri.

Nikaweka frying pan jikoni na kuweka mafuta vijiko 3 vikubwa, yalipo pata moto nikaweka mayai nikakaanga hadi yalipo iva, nikatoa na kuweka kwenye sahani, omellete ikawa tayari.

Kisha nika gawa omellete ktk vipande 4, nikapasha mikate ya burger ktk microwave Kwa sekund 30. Kisha nikaweka Kipande 1 cha omellete kwenye mkate wa burger (kile Kipande cha chini) na juu yake nikaweka slice of fresh tomato na ketchup, Kisha nika malizia kuweka kipande cha juu cha mkate wa burger, na omellete burger yetu ikawa tayari kuliwa Kwa lunch, #karibuni.