ROSTI LA BAMIA NA BILINGANYA

Rosti la bamia na bilinganya, jamani ndio hizi video yk niliyo post Jana.
Hapa zimeshaiva, na kukolea nyanya hatari.

πŸ‘‡πŸΏ
Bamia bilinganya rosti recipe
.
Bamia robo kilo
Bilinganya 1 kubwa
Kitunguu 1 wastani
Nyanya 8 kubwa (nili saga kwenye blender)
Chumvi kijiko 1 kidogo
Mafuta ya kupikia (kadiria kutokana na matumizi yako)
.
Jinsi ya kuandaa na kupika
.
Niliosha bamia, bilinganya, kitunguu na nyanya. Kisha nika kata kila kitu vipande vya wastani kasoro nyanya.
.


Niliweka mafuta ktk sufuria na kuwasha jiko, yalipo pata moto, nikatia kitunguu nika kikaanga kidogo, Kisha nikatia bamia na bilinganya nazo nikazi acha kigodo zijikaange kwenye mafuta, Kisha nikaweka nyanya na chumvi, nikafunika na mfuniko. .
Nikaacha vichemke hadi mchuzi wa nyanya ulipo anza kukaukia, nika geuza na mwiko kisha nikaacha jikoni Kama dk mbili, nikazima jiko na kuweka sufuria pembeni.
.
Rosti letu la bamia na bilinganya likawa tayari , mi nili kula na ugali na nyama choma wenzangu walikula wali. Nakuja kukumbuka sijapiga picha tayari tumeanza kula ☺️..
πŸ‘‡πŸΏ
Kupata ratiba ya chakula ya mwezi mzima, ipo ktk soft copy tsh 10,000 Whatsap 0752 741 831.

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started