JUICE YA UKWAJU MIX NA UBUYU

Juice ya ukwaju mix na ubuyu 🍹(tamarind baobab juice) kama hujawahi kunywa mchanganyiko wa juice hii basi uhondo una kupita. Ni juice(mix) tamu sana hasa ukila na nyama choma.
.

Mahitaji

ukwaju nusu kilo

ubuyu robo kilo

asali vijiko vikubwa 5

maji ya moto lita

Jinsi ya kutengeneza

Baada ya kutoa vyote kwenye maganda yake ni nika loweka ukwaju na ubuyu kwenye maji ya moto (maji niliweka lita 2). Nikauacha kwenye maji hadi maji yalipo poa kabisa, nikachukua mwiko na kuanza kukoroga ili ubuyu na ukwaju utoke kwenye maganda yake. Kisha nikachuja na kuweka asali na nikaweka juice Yangu kwenye fridge ipate baridi.
#Karibu

tembelea piaπŸ‘‡πŸΏ

https://eunicemahundi.wordpress.com

Ujifunze ujasiriamali

Published by eunicemahundi

HiπŸ™‹πŸΎ, Naitwa Eunice Mahundi, ni #foodblogger na napenda sana mapishi, wengi mna nifahamu kama Mjasiriamali Ila food blogging ni kitu kingine nacho kipenda sana. 🍲🍝🍹🍷🍚🍽 Mapishi Yangu huwa ni simple, Ila yanavutia na mengi ni swahili cuisine, pia huwa napost dondoo za jikoni kama; -Usafi -vyombo -ratiba ya chakula/mapishi -nk Karibu sana na ione malkia wa jiko blog kama nyumbani kwako, ujifunze mengi. Ukiwa na maswali, maoni au chochote kile wasaliana nami: πŸ“§ eunicemahundi@yahoo.com Whatsapp : 0752 741 831or 0657 234 897

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started